
Gurudumu la Uchumi
Podcast af RFI Kiswahili
Begrænset tilbud
1 måned kun 9 kr.
Derefter 99 kr. / månedIngen binding.

Mere end 1 million lyttere
Du vil elske Podimo, og du er ikke alene
Bedømt til 4,7 stjerner i App Store
Læs mere Gurudumu la Uchumi
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Alle episoder
145 episoderMkataba wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani maarufu kama AGOA umefika tamati, ni mkataba uliokuwa unatoa fursa kwa nchi za Afrika kufikia soko la Marekani bila vikwazo vya kiushuru, bara hili likitengeneza faida ya mabilioni ya dola kupitia mkataba huu, hata hivyo kukoma kwake tayari kunashuhudiwa athari yalke kwenye baadhi ya nchi, kuanzia katika viwanda vya nguo nchini Kenya hadi kwa wasafirishaji huko Ghana, maisha ya watu walioajiriwa kupitia mkataba huu yako mashakani.
Msikilizaji katika nchi zote za Afrika Mashariki, kuna wimbi jipya la matamanio kuhusu hali ya biashara, vijana, wakiongozwa na ubunifu na ustahimilivu! Wakigeuza harakati zao kuwa biashara zinazostawi, kubadili changamoto kuwa fursa na ndoto kuwa ukweli. Tutazungumza na Andrew Lukuwi, yeye ni mjasiriamali kijana akiwa nchini Tanzania, pamoja na Dr Onesmo Kyauke mchambuzi wa masuala ya uchumi na siasa akiwa Tanzania.
Kulingana na ripoti ya umoja wa Afrika, bara hilo linapoteza takribani dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka kupitia njia zisizo halali kama ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, utoroshaji wa mali na mitaji na udanganyifu kwenye biashara. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza, Kwanini hali hii inaendelea licha ya uwepo wa sheria kali? Nani anafaidika? na nini kifanyike kuzuia upotevu huu mkubwa wa rasilimali fedha? Tutakuwa na wataalamu Walter Nguma na Dr Ponsian Ntui.
Leo hii tunatupia jicho uchumi wa bluu, eneo la kiuchumi linalotajwa kama suluhisho jipya la maendeleo endelevu, kukuza ajira na ubunifu, hata hivyo chini ya uso wa maji, maswali magumu yanajitokeza: Je, tunawekeza kimkakati kwa kuzingatia pia jamii zinazozunguka maeneo haya? Tutazungumza na Dr Ponsian Ntui mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini mwanza nchini Tanzania, maarufu kama SAUT.
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunazungumzia mabadiliko makubwa ya kiuchumi kuhusu namna malipo ya kidijitali yanavyochochea huduma jumuishi za kifedha, ukuaji wa uchumi, na mageuzi ya kidijitali kwenye nchi za Afrika. Wageni wetu leo ni Ali Mkimo mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, pamoja na Lucy Nshuti Mbabazi, mkurugenzi wa taasisi ya Better Than Cash Alliance iliyochini ya shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP.

Mere end 1 million lyttere
Du vil elske Podimo, og du er ikke alene
Bedømt til 4,7 stjerner i App Store
Begrænset tilbud
1 måned kun 9 kr.
Derefter 99 kr. / månedIngen binding.
Eksklusive podcasts
Uden reklamer
Gratis podcasts
Lydbøger
20 timer / måned

































