Billede af showet Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Podcast af United Nations

swahili

Nyheder & politik

Begrænset tilbud

1 måned kun 9 kr.

Derefter 99 kr. / månedOpsig når som helst.

  • 20 lydbogstimer pr. måned
  • Podcasts kun på Podimo
  • Gratis podcasts
Kom i gang

Om Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Alle episoder

4620 episoder

Billede af episoden 24 JULAI 2026

24 JULAI 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani kwa Maendeleo Endelevu awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kupitia Ofisi ya Rais inayohusika na Maendeleo ya Vijana, limeendelea kutumia mafunzo ya ufundi stadi kama njia ya kudumisha amani na kuwajengea uwezo vijana kiuchumi. Hii ni katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiwemo namba moja la kuondokana na umaskini na namba 16 linalolenga pamoja na mambo mengine kujenga amani kwenye jamii.Rashid Malekela, balozi kijana wa UNDP Tanzania alihudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Wanawake, UN Women, limeonya kuwa wanawake na wasichana katika mji wa El Obeid nchini Sudan sasa wanakabiliwa na hatari mbili wanapokwenda kuchota maji ambayo ni mashambulizi ya droni mchana yanawalazimu kusubiri hadi usiku, ambako hukumbana na ubakaji na ukatili mwingine wa kingono.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema kuwa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 130,000 nchini Burundi, wengi wao wakitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRc unaweza kusitishwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu endapo halitapata ufadhili wa haraka.Na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO, umefanikiwa kurejesha utulivu katika eneo la Nyakunde jimboni Ituri, hatua iliyowezesha kurejea kwa harakati dhidi ya ugonjwa wa Ebola.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

I går - 9 min
Billede af episoden 22 JULAI 2026

22 JULAI 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Huko DRC madini ya kimkakati mashariki mwa nchi yamekuwa kichocheo cha mizozo. Mgeni wetu leo pamoja na mambo mengine anaangazia jinsi vita imezuia wao kuendelea na uchimbaji madini. Yeye anaishi Goma, lakini Salama Machaano, wa redio washirika wetu, Adventista World Radio, Tumaini Mkuu iliyoko Bukavu, jimboni Kivu Kusini alifnga safari hadi Goma kuzungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu “Utawala wa rasilimali za asili: Msingi wa amani, usalama na ustawi” chini ya kipengele cha ajenda ya “Kudumisha amani na usalama wa kimataifa.” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao hicho ameeleza vipaumbele vinne kuwa ni kuhakikisha manufaa ya haki yanapatikana kutokana na rasilimali za asili, kuimarisha uwazi na ushirikiano ili kukabiliana na biashara haramu, kukuza utatuzi wa amani wa migogoro inayohusiana na rasilimali, na kuzingatia masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika kuzuia migogoro na kujenga amani.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetoa wito wa kulindwa kwa raia na kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu kuwafikia wenye uhitaji nchini Sudan baada ya shambulio lililotekelezwa juzi tarehe 20 Julai kwa kutumia ndege zisizo na rubani likilenga soko la Ar Rahad katika jimbo la Kordofan Kaskazini na kusababisha vifo vya watoto wawili na kuwajeruhi wengine sita.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kusikitishwa sana na taarifa kwamba makumi ya wahamiaji wamefariki dunia au hawajulikani walipo kufuatia kuzama kwa meli katika pwani ya Mauritania, ambapo tarehe 18 Julai manusura 38 waliokolewa na Walinzi wa Pwani wa Mauritania karibu na mji wa Nouadhibou walipokuwa wakijaribu bahati yao kuelekea nchini Hispania. IOM kupitia Mkurugenzi wake wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Sylvia Ekra, imesema watu wanaendelea kuhatarisha maisha yao kwa sababu zinazowasukuma kuondoka katika nchi zao bado zipo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

22. juli 2026 - 9 min
Billede af episoden 21 JULAI 2026

21 JULAI 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Jana katika moja ya viunga vya jiji la Nairobi, wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na raia wa Afrika Kusini na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Kenya, ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela walikitembelea Kituo cha Kulelea Watoto ya Yatima kinachofahamika kwa jina Serah’s Vision Children’s Home na walikaa kituoni hapo kwa dakika 67.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Ikiwa ni miezi tisa tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas, hali ya usalama kwa raia wa Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel inaendelea kuzorota. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imesema hii leo kuwa hakuna eneo linaloweza kuchukuliwa kuwa salama kwa Wapalestina, huku Wizara ya Afya ya Palestina ikiripoti kuwa zaidi ya watu 1,100 wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel tangu Oktoba mwaka 2025.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limeonya kuhusu hatari ya safari za baharini kuelekea barani Ulaya kupitia bahari ya Atlantiki baada ya watu 144 kuripotiwa kufariki au kutoweka katika pwani ya Mauritania wiki iliyopita. Katika tukio la hivi karibuni watu 387 waliokolewa katika operesheni za uokoaji.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO linasema licha ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola wa virusi aina ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuendelea kuenea kwa kasi, baadhi ya maeneo yanaanza kuonesha dalili za hali kutengamaa kutokana na hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huo.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

21. juli 2026 - 11 min
En fantastisk app med et enormt stort udvalg af spændende podcasts. Podimo formår virkelig at lave godt indhold, der takler de lidt mere svære emner. At der så også er lydbøger oveni til en billig pris, gør at det er blevet min favorit app.
En fantastisk app med et enormt stort udvalg af spændende podcasts. Podimo formår virkelig at lave godt indhold, der takler de lidt mere svære emner. At der så også er lydbøger oveni til en billig pris, gør at det er blevet min favorit app.
Rigtig god tjeneste med gode eksklusive podcasts og derudover et kæmpe udvalg af podcasts og lydbøger. Kan varmt anbefales, om ikke andet så udelukkende pga Dårligdommerne, Klovn podcast, Hakkedrengene og Han duo 😁 👍
Podimo er blevet uundværlig! Til lange bilture, hverdagen, rengøringen og i det hele taget, når man trænger til lidt adspredelse.

Vælg dit abonnement

Mest populære

Begrænset tilbud

Premium

20 timers lydbøger

  • Podcasts kun på Podimo

  • Ingen reklamer i podcasts fra Podimo

  • Opsig når som helst

1 måned kun 9 kr.
Derefter 99 kr. / måned

Kom i gang

Premium Plus

100 timers lydbøger

  • Podcasts kun på Podimo

  • Ingen reklamer i podcasts fra Podimo

  • Opsig når som helst

Prøv gratis i 30 dage
Derefter 129 kr. / måned

Prøv gratis

Kun på Podimo

Populære lydbøger

Ofte stillede spørgsmål

Flere spørgsmål og svar
Kom i gang

1 måned kun 9 kr. Derefter 99 kr. / måned. Opsig når som helst.