
Gurudumu la Uchumi
Podcast de RFI Kiswahili
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Empieza 7 días de prueba
$99.00 / mes después de la prueba.Cancela cuando quieras.
Todos los episodios
134 episodios
Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.

Alhamisi ya Juni 12, nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa pamoja kupitia Mawaziri wa Fedha, waliwasilisha Bajeti ya mwaka wa fedha ya mwaka 2025/26. Waziri wa fedha John Mbadi aliwasilisha Bajeti ya Shilingi za nchi hiyo Trilioni 4.2. Bajeti ya Tanzania kwa mwaka huu wa fedha ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 56.49 huku Bajeti ya Uganda ikiwa ni Shilingi za nchi hiyo Trilioni 72.3. Lakini bajeti hii ina maana gani kwa raia wa nchi hizo na je bajeti hizi zinatoa taswira halisi ya mikakati yao nchi hizo kujitegemea na pia kukua? Skiliza makala haya upate ufahamu zaidi tukizungumza pia na David Otieno, mtafiti wa masuala ya bajeti kutoka shirika la Amnesty International.

Wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili namna teknolojia inaweza kutumika katika kukifanya kilimo kuwa cha kisasa. Tumezungumza na Mhandisi Octavian Lasway, mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na umwagiliaji.

Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii tunajadili namna mfumuko wa bei na mzigo wa madeni umeendelea kuziathiri nchi zinazoendelea na namna gani zinaweza kukabiliana na changamoto hii.

Msikilizaji wiki iliyopita katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tulianza na sehemu ya kwanza ya mada kuhusu namna teknolojia inavyoweza kuhusihwa kwenye biashara kutatua changamoto zinazolikabili bara la Afrika, ikiwemo biashara ya kidijitali kuchochea utangamano, kuongeza ufanisi na kuleta maendeleo. Leo nakuletea sehemu ya pili ya mazungumzo yangu na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Empieza 7 días de prueba
$99.00 / mes después de la prueba.Cancela cuando quieras.
Podcasts exclusivos
Sin anuncios
Podcast gratuitos
Audiolibros
20 horas / mes