Siha Njema
Taratibu hizo za pamoja yatahakikisha kuwa nchi za Afrika zinaweka bajeti kwenye sera ya uchumi na kuipa kipau mbele ufadhili wa afya
Vær den første til å kommentere
Registrer deg nå og bli medlem av Siha Njema sitt community!
99 kr / Måned etter prøveperioden. · Avslutt når som helst.
226 Episoder
Majanga yanaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa watoto
Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama Hali hii imewasababisha changamoto za afya ya akili anavyoeleza mwaandishi wetu Petronila Ogalo.
Mwendelezo wa mlipuko wa Ebola DRC na namna wenyeji wanavyojikinga
Watu 220 wamefariki kwenye mlipuko wa Ebola unaohusishwa na virusi adimu vya Bundibugyo huku wengine zaidi ya 1000 wakiwa wameambukizwa Mlipuko huu hatari umesababisha baadhi ya mataifa kufunga mipaka yake na kuweka masharti magumu ya tahadhari
Kwenye kapu la sekta ya afya kufuatia kongamano la Africa Forward
Baadhi ya makubaliano yalitotangazwa na Ufaransa baada ya siku mbili ya kongamano la Africa Forward ni ufadhili kwa uzalishaji wa dawa na chanjo hapa barani Afrika. Shirika la Unitaid pia lenye ushirikiano na Ufaransa lilitangaza kuratibu mchakato wa kuzalishwa dawa mpya ya kuzuia virusi vya HIV ,Lenacapavir kuzalishwa Afrika Kusini. Na kwenye viungo vingine vilivyosheheni majadiliano ya kuimarisha mifumo ya afya Afrika ni kilimo endelevu .
Mashirika ya kiraia Afrika yanataka nchi za Afrika kuwa na taratibu za pamoja kudhibiti magonjwa
Watalaam wasisitiza uwekezaji wa utafiti wa DNA barani Afrika
Utafiti unaoangazia vinasaba katika ukanda wa Afrika unaweza kuwa jawabu kwa ubainishaji potovu,gharama ya juu ya matibabu na usugu wa vimelea . Kwa kuanzia , Mashirika matatu ya Afrika ya kitafiti yametangaza mkataba wa dola milioni 3 nukta 5 ambao utawekezwa kwenye utafiti huu wa DNA barani . Mashirika haya yakiwa ni Biolinx Africa, YTO Foundation yenye makao Ivory Coast na Nextgen Molecular Lab nchini Kenya.
Kommentarer
0Vær den første til å kommentere
Registrer deg nå og bli medlem av Siha Njema sitt community!