
Suaheli
Kostenlos bei Podimo
Starte jetzt und verbinde dich mit deinen Lieblingspodcaster*innen
Mehr Gurudumu la Uchumi
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Ushindani wa mataifa makubwa na mustakabali wa uchumi wa Dunia
Msikilizaji mataifa makubwa kama Marekani, China, Urusi na Ulaya yanaendelea kushindana kiuchumi, kuanzia kwenye biashara, teknolojia, nishati na rasilimali. Lakini je, ushindani wao unaathiri vipi uchumi wa dunia? Leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi tunajadili, “Athari za Kiuchumi kwa Dunia Zitokanazo na Ushindani wa Maslahi ya Kiuchumi kati ya Mataifa Makubwa.”
Kenya Kuwa Singapore ya Afrika: Ndoto au Uhalisia?
Msikilizaji Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kusisitiza azma ya kuifanya nchi yake kuwa Singapore ya Afrika, suala ambalo limeibua mjadala mkali nchini humo baadhi wakisema ni suala ambalo halitawezekana chini ya utawala wake na wengine wakiona ni jambo linalowezekana. Kwenye makala yetu leo tunajiuliza, je, Kenya inaelekea huko? Ndoto hii inawezekana au ni siasa?
Kutoka Ufugaji wa Mifugo hadi Samaki: Mabadiliko ya Kiuchumi Kajiado
Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.
Sherehe za mwisho wa mwaka zisikuache bila pesa, fahamu mbinu za kudhibiti matumizi yako.
Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyabiashara.
Ripoti ya Oxfam-Kenya: Uchumi unakua, lakini Wakenya wengi ni masikini, kwa nini?
Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya. Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?